Zaidi ya shule ishirini (20 ) zime lazimika kufunga milango yake katika vijiji mbali mbali katika secta ya Bapere kutokana na mashambulizi ya mara kwa amara inayo tekelezwa na watu wanao dhaniwa kuwa ADF japo operesheni za muungano wa kijeshi unao endelea eneo hilo kwa sasa .
Waalimu wa shule wametangaza hii juma tatu kumi na sita wakati wa siku yam toto wa Africa wazazi kama vile waalimu wakilaumu serikali kushindwa kulinda wananchi japo malalamiko ya mara kwa mara ,vijiji vikishambuliwa kila siku na watu wanao kuwa na silaha ambao serikali inasema ni watu kutoka kundi la ADF.
Watoto wa shule wakikasirishwa na hali ya ukosefu wa usalama ambayo imedumu kwa muda mrefu katika uangaliza wa viongozi wa serikali n ahata Umoja wa Matifa yaani MONUSCO DRC ambao hutangaza mara kwa mara kuwa wamekuja DRC kuwalinda raia dhidi ya ukiuwakwaji wa haki na misingi ya binaadamu.
Utafaahmu kwamba idadi kubwa ya Watoto eneo la secta ya Bapere na Mangurudjipa Watoto wengi wame lazimika kuanza shughuli za uchimbaji madini kutokana na ukosefu wa shule na waalimu wengi wakikimbiia vijiji vya mangurudjipa kuhufia usalama wao. Wakaazi na mashirika ya kiria iki lalaka kwa muda muda mrefu bila mafanikio hadi sasa.