Akiwa ziarani katika Mji wa Kibumba wilayani Nyiragongo Mkoani Kivu Kaskazini ,Eraston Musanga gavana wa Kivu Kaaskazini eneo linalo dhibitiwa na M23 asema wakaazi wa Kibumba wilayani Nyiragongo wamepitia mateso kwa muda mrefu nae neo lao liliikaliwa kwa muda mrefu na wapiganaji wa FADLR kutoka Rwanda ambao walikaa kwa muda mrefu katika Mbuga la wanyapori la Virunga.
Musanga ameomba wakaazi hawa kushirikiana na vyombo vya usalama katika ulinzi na usalama wa wanavijiji ambao kwa sasa washuhudia usalama ambao waombwa kudumu Zaidi,Musanga amezungumuza na vijana ,wasichana wanawake na wazee wa Kibumba ,kilometa Zaidi ya ishirini kaskazini mwa Mji wa Goma,ikiwa vilevile karibu na Mpaka wa Rwanda na DRC ambako wakaazi wake wote ni wakulima na wafugaji.
Hii ikiwa ni mara ya kwanza kiongozi huyu kutembeleea wakaazi ambako alitembelea hata hivyo hospitali ambazo zakabiliwa na tatizo la vifaa vingi na wakaazi wakiwa hana uwezo wakulipa hospitali kutokana na maisha magumu waliio pitia katika kambi za wakimbizi kabla ya kurudia Nyumbani.
Kuhitimisha ziara yake Eraston Musanga ameomba wananchi kuacha ukabila ambao ni tatizo kubwa katika maendeleo na kusababisha mgawanyiko kati ya watu .