Baada ya kutwigwa maswali na wakaazi wa mugunga siku zilizo pita Gavana wa Kivu Kaskazini upande unao dhibitiwa na M23 Erasto Musanga Bahati ametembelea kituo kinacho jengwa kwa ajili ya kupokea umeme kutoka Ethiopia umeme ambao utasaidia mataifa mengi Africa Mashariki kila taifa ikiwa na kituo chake,Mjini Goma Kazi za ujenzi na kuweka vifaa muhimu zikiendelea .Eraston Musanga Bahati asema .
Mkuu wa SNEL Denis munyangi ikiwa kiongozi wa secta ya serikali inayo husika na umeme Kivu Kaskazini asema mradi huu ni muhimu kwa eneo hili ambalo kwa muda mrefu secta ya umeme imekuwa bishara kubwa na wakaazi kushindwa hata kupata huduma nzuiri ila mradi huu utasaidia sana kuboresha masha ya wananchi wa DRC hasa eneo lake la Mashariki .
Utafahamu kwamba uzinduzi wa mradi wa umeme huo utazinduliiwa Septema elfu mbili ishirini na tano Mjiwa Goma ukiwa utapokea tisini na tatu point inane (93,8) Mega Wats itakayo saidia sehemu kubwa ya mashariki mwa Congo ikiwemo Bukuavu kupitia kiwanda kitakacho wekwa Bwandanda ,kukiwa na mpango wakuelekea Bunia Mkoani Ituri.
IR wa mradi huo asema mradi huo wakuleta umeme DRC unasaidiwa na serikali ya Ujeremani ,mradi unao garimu milioni Tisa ya Dola za marekani.
Wachambuzi wakiomba serikali ya Congo DRC nayo kujaribu kutumia pesa za serikali katika ujenzi wa taifa lake kuliko watu Binafsi kujibikizia pesa ambazo ni pesa za uma ,kwani Congo ina mito nyingi ambayo yaweza zailisha umeme Zaidi kuliko hata huu kutoka Ethiopia ila ikiwa ni kwa viongozi kupenda taifa lao.