Evariste somo amesema alitembelea lubero kutazama miradi ya maendeleo inayo tekelezwa na serikali ya Kinshasa .Eneo la magharibi mwa wilayani hiyo kukiwa mgomo eneo la bapere kufatia mauaji na mashambulizi ya watu wanao dhaniwa kuwa ADF.
Viongozi wa kijadi eneo la mangurudjipa wakiendelea na mgomo wa kazi ulio anza juma tatau iliopita kutokana na mauaji ya watu Zaidi ya arbaini katika vijiji mbali mbali katika secta ya bapere wilayani Lubero. Wakaazi eneo hilo wakishutumu serikali kuwa na uzembe katika operesheni za kijeshi dhidi ya ADF
Operesheni za kijeshi wilayani na Lubero zikiwa zimefanya siku nyingi na watu kuendelea kushambuliwa na kuwawa Pamoja na makaazi yao kuchomwa moto ,na kusababisha vijiji vingi kubaki bila wakaazi na kuota majani