Wkaati ambapo pande zinazo husika katika mzozo mashariki mwa Congo zikiombwa kurudi kwenye meza ya mazungumuzo huko Doha Qatar mapigano bado yaendelea katika vijiji mbali mbali kama eneo la Kalungu wilayani Mwenga ,inayo kuwa eneo Itombwe .mapiganao inayo pelekea watu wengi kuwa na wasiwasi Kivu Kusini nakuomba pande husika kusitisha mapigano kwani wakaazi bado waendelea kukimbia vijiji vyao kukiwa mvua kali.
Jeshi la serikali na M23 bado wakiendelea kushutumiana kila mmoja ,wapiganaji wazalendo nao wakiombwa kuheshimu amri ya usitishwaji wa mapigano ilio afikiwa huko Doha kati ya pande husika katika mzozo wa DRC ,mzozo ambao umekuwa na wahusika wengi katika kanda ya maziwa makuu na Africa mashariki kama vile Africa kusini.
Wataalaamu wa mizozo wakiomba mzozo wa DRC kutatuliwa kwa mazungumuzo kuliko utumiaji wa silaha .mzozo wa DRC hasa unao fatia mapigano Kivu Kusini waweza igusa taifa la Burundi ambalo waasi wasema linaunga mkono wapiganaji wa FDLR na serikali ya Congo DRC.mapigano kati ya M23 na serikali eneo la kamanyola itakuwa hatarishi kubwa kwa Mji wa Bujumbura iwapo hakuna suluhisho la kidiplomasia kwani Mji wa Uvira ni muhimu kwa usalama wa Burundi wasema waataamu wa kiusalama maziwa makuu na Africa mashariki ambao wasema huenda mzozo wa DRC kugeukia Burundi.