DRC/

Mashirika ya kiraia wilayani Beni ya toa tadhari kwa kwa viongozi kuhusu uwepo wa watu wanao dahniwa kuwa ADF katika mashamba za watu

AGUSTI 20, 2025
Border
news image

Baada ya mashambulizi na kuchoma makaazi ya watu katika Mji wa OICHA wilayani Beni ,mashirika ya kiraia eneo husika ya laumu vyombo vya usalama kupuuza taarifa kutoka wakaazi ,kwani tukio la mauaji ya hivi karibuni lilifanyika baada ya shirika za kiraia na wakaazi kulalamikia uwepo wa ADF katika mashamba za watu.

Isac Kavalami mkuu kiongozi wa shirika la kiraia katika mji wa Oicha asema mauaji ya watu na kushambulia makaazi ya watu ,inasikitisha sana ,kwani viongozi husika waliambiwa kuhusu uwepo wa waasi hao.kuwawa kwa wakaazi Zaidi ya nane akiwemo mtoto mmoja na polisi wa serikali ni sikitiko asema ISAC ,(( tumeshambuliwa kila siku,wakulima walikuwa wameanza kulima shamba zao lakini leo kwa kweli tuna shangaa sana kuona tena watu wana shambuliwa ,tunaomba jeshi la serikali na UPDF kuweka nguvu Zaidi,na kushirikisha wakaazi katika usalama kwani ,wakati mmmoja twa shakia baadhi yaw ana usalama )).

Jeshi la serikali ya Congo mara kwa mara ikiomba wakaazi kushiirikiana na vyombo vya usalama katika kuwapa taarifa ,wengi wakijiuliza kwanini ndege za kivita ama drones za serikali hazitumiwi katika operesheni dhidi ya ADF japo zilitumiwa kutwangana na M23.

Mauaji ya ADF ikiwa ikefanya miaka Zaidi ya kumi hadi sasa kukiwa malefu ya waatu kuhama makaazi yao na wengine kuppoteza maisha.

MTV1