Timu za kiufundi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Jamhuri ya Rwanda zilianzisha maandishi ya Mkataba wa Amani mnamo Jumatano, Juni 18, 2025, huko Washington, D.C.
Maandishi hayo yalitiwa saini mbele ya Katibu Chini wa Masuala ya Kisiasa wa Marekani Allison Hooker, kwa ajili ya maandalizi ya kutia saini makubaliano ya amani mnamo Juni 27, 2025.
Hayo yametangazwa katika taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.
Hubert Masomeko mchambuzi wa maswala ya kiusalama maziwa Makuu asema mkataba huo ni muhimu zaidi kumaliza uhasama ulieko kati ya Rwanda na DRC kwani hii ya wachanyikisha wanainchi wa mataifa hayo mawili .
Masomeko anasema uhusiano kati ya Rwanda na DRC utaweza kupunguza tension kubwa ilieko maziwa makuu kwani vita vya Congo vya weza zagaa maziwa makuu na Africa mashariki .
Huku kukiwa wasi kuhusu ujio wa waasi waa AFC/M23 ambao nao wako katika mazungumuzo na serikali ya kinshasa Doha Qatar.