RDC

SADC yaendelea kuwaondoa wanajeshi wake Mjini Goma Kivu Kaskazini mashariki mwa DRC.

JUNI 23, 2025
Border
news image

Zaidi ya wanajeshi 461 wa SADC waliondoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kurejea katika nchi zao za asili, kupitia Rwanda,Akizungumuza na wakaazi wa kata la Bujovu mpakani mwa Rwanda na DRC Kanali Jimmy Nzamuye alisema wanajeshi hao wanarudi nyumbani kwao baada ya kushindwa mapigano na kutekwa na M23 ambao wameachiliwa katika mikataba ya kuheshimu haki na msingi ya binaadamu.

Miongoni mwao walikuwa wanajeshi 317 wa Afrika Kusini na wanajeshi 144 kutoka Malawi.huku kukiwa bado idadi ndogo inayo baki wkaiwemo makamanda wao ambao bado wapo Mjini Goma wakisubiri utaratibu mwengine wakurudi nyumbani kwao kupitia Rwanda Tanzania.

M23 ilisema kuwa SADC walikuwa miongoni mwa watu walaio ungana na jeshi la Congo FARDC kupambana nao na haiwezi kubalika wabaki Mjini Goma wakiwa na silaha Pamoja na kuendelea na majukumu yao ,muhimu na kuondoka kupitia barabara wakitumia Taifa la Rwanda na baadae Tanzania wakihakikisha kwamba wanarudia kwao Nyumbani salama.

Wananchi wa DRC hasa kutoka mashariki mwa Congo wamekuwa wakiomba serikali ya Congo kujenga jeshi lake kuliko kupoteza mud ana pesa kutafuta mamluki ambao hutumia pesa ambazo zaweza jenga taifa na miradi nyingine za maendeleo.SADC inaondoka DRC kwakupisha mazungumuzo kati ya Rwanda na DRC kwakumaliza uhasama kati yao.

MTV1 Online