RDC
Tom Fletcher, Mratibu wa Misaada ya Dharura, UN amewasili Goma leo hii.Mratibu huyu ata tembelea eneo nyingi ikiwemo Shasha,Minova na bwerema pamoja na nyiragongo ambako amekuja kutasmini hali ya kiutu
JUNI 25, 2025
Kiongozi huyu amewasili eneo linalo dhibitiwa na M23 ili kuandaa misaad kwa ajili ya wakaazi walio kimbia vijiji vyao na kuwa wakimbizi wa ndani lakini kwa sasa wamrudi manyumbani baada ya Goma kuchukuliwa na M23 na kambi zote kuondolewa.
Wakaazi wengi wamerudi nyumbani kwao ila wakihitaji kunishinikiza watu walio ppoteza vitu vyao na makaazi yao ikiwa haipo tena baada ya kushambuliwa ama kuanguka kutokana na kuachwa muda mrefu kwenye vijiji.
Wakaazi wasema ujio wa viongozi hao inaonesha kwamba Umoja wa Matifa unatambua kwamba eneo linalo dhibitiwa na M23 lina watu ambao vile wana hitaji huduma na maisha kama vile eneo linalo dhibitiwa na serikali ya Kinshasa.