Akizungumuza na MTV 1 ONLINE Constan Same Bangalwa mwanahabari katika Mji wa bunia mkoani ITURI asema kwa sasa wakaazi wa Aru hasa vijiji vya kakwa washuhudia hali mbaya ya joto kali yaani ukame ambao umeonekena kwa hali ya juu .
Ukame unao sababisha mifugo na wanya pori kukosa chakula na mimea kwa wakulima kukauka kwa ghafla na kuathiri vijiji kadhaa katika eneo la Aru, vilivyoko zaidi ya kilomita 300 na mji wa Bunia mkoani Ituri.
Taarifa kutoka shirika za kiraia eneo hilo zasema hali ni mbaya na lazima serikali kuchukuwa hatua ya kusaidia wakaazi wa eneo hilo ambao kwa sasa wakabiliwa na njaa na wengine wakionekana sasa na utapia mulo.
Eneo la kakwa likiwa ndilo limeathirika sana zaidi kuliko vijiji vingine asema Constan Same Bangalwa mwanahabari kutoka Bunia sababu kubwa ikiwa mabadiliko ya hali ya hewa. Visima vya maji vikiwa vimekauka na hivyo kufanya upatikanaji wa maji kuwa mgumu kwa wakazi.
Uhaba huu wa maji pia una athari za moja kwa moja katika kilimo na ufugaji wa mifugo, shughuli mbili muhimu kwa maisha ya jamii na wakaazi wa eneo husika.