DRC

Viongozi wa jeshi la Congo FARDC walionya jeshi kuheshimu haki na misiingi za binadamu

juni 11, 2025
Border
news image

Serikali ya kinshasa imeanza maafunzo mapya na idelojia mpya kwa jeshi lake hasa wale wanao pata upya mafunzo na wanao kimbia uwanja waa mapigano mashariki mwa Congo .

Wakuu wa FARDC waaomba jeshi kulinda nidhamu na kukomesha tabia ya uporaji na ubakaji wa wananchi wake inayo ripotiwa dhidi yao ,

Siki zilizo pita baadhi ya wanjeshi wa serikali walihukumiwa vifungo mbali mbali baada ya uporaji na wizi katika mji wa Kimbulu wilayani Lubero ambako walipora nyumba za watu na kubaka wanawake .

Huku viongozi wa kijeshi wakiamua kuwachukulia hatua askari wote atakae kiuka maagizo ya viongozi, Hii ikiwa hatua ilio chukuliwa Katika Kituo cha Mafunzo cha Makomandoo cha FARDC kilichoko KOTA KOLI (Kaskazini - Ubangi),

Kanali Yav MAJITA Charles, Kamanda Dir 22 SECAS, mwishoni mwa Mei alitoa ufahamu kwa wafunzwa makomandoo wa FARDC kuhusu maadili na taaluma ya Jeshi ili wawe na ujasiri pamoja na kuheshimu haki za binaadamu wakitumikia wananchi.

Askari wengi waliwasili eneo hilo kutoka kivu Kaskazini ambako walikabiliana na M23 ambayo kwa sasa imesha chukuwa miji ya Goma na Bukavu mashariki mwa congo DRC.

AM/MTV News DRC