Delio Kimbulungu ni kutoka Kundi la waasi wa AFC/M23 ambae alisoma Taangazo na hatua ilio chukuliwa na waasi wa AFC/M23 kuweka viongozi wapya ambao wameteuliwa siku chache baada ya alie kuwa gavana wa Mkoa huo upande wa M23 kupewa kazi nyingine kwa mjibu wa kundi hilo.
Kuteuliwa kwa gavana mpya wa Upande waa M23 mkoni Kivu Kusini je utachangia nini kwa wakaazi ama kwa usalama wa Mkoa wa Kivu Kusini ,tumezungumuza na gavana alie tauliwa ambae amesema atafanya kazi kufatia maagizo ya viongozi wake na kuhakikisha anashirikiana na wakaazi wa Mkoa wa Kivu Kusini mji mkuu ukiwa Bukavu.
Hatua hii imechukuliwa siku chache baaada ya Muwakilishi wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa nchini DRC yaani Mkuu wa MONUSCO kuhitimisha ziara yake Mjini Goma ambao alifanya siku tatu baada ya kukutana na vingozi wa AFC/M23 .
M23 ikiwa na sehemu kubwa ya mkoa wa Kivu Kaskazini na Mkoa wa Kivu Kusini na sehemu ndogo bado ikibaki katika mikono ya serikali ya Kinshasa wakisubiri mazungumuzo ya Doha Qatar kwa ajili ya kutafuta na usalama kwa njia isio ya utumiaji wa silaha.