RDC
Wanaharakati wakutetea haki za binaadamu wilayani Lubero waomba serikali ya DRC kuwachukulia hatua watu wenye silaha walio husika katika ubakaji wa wanawake
JUNI 23, 2025
Shirika zenyi kutetea haki zabinaadamu zasema kuliripotika idadi kubwa ya wanawake walio bakwa na watu wenye silaha wilayani Lubero wakati wa Maapigano ulio kuwa ikiendelea kati ya M23 na jeshi la serikali linalo saidiwa na vijana wazalendo ,Hospitali mbali mbali zili wapokea wanawake walio bakwa kutoka vijiji vya masereka,kipese ,Kitsombiro na vijiji vingine .
Wengi wao walipelekwa katika Mji wa Butembo na musienene ambako walisaidiwa na wengi wao wakiambukizwa ukimwi na magonjwa ya ziinaa,shirika hizo zimeomba hatua kali kuchukuliwa kwa viongozi na wanajeshi walio husika katika vitendo vya ubakaji wa wanawake ambao wali zalilishwa na kutendewa unyama na watu wenye silaha wakibakwa.