Wakaazi walio kubali kuzungumuza na MTV 1 wasema milio ya risasi imeshuhudiwa katika kata ya Bagira ambako wapiganaji wazalendo walikuja na kurushiana risaisi vikali na waasi wa M23 ,ambako mkaazi huyu alie hifadhi jina lake asema kata nyingi zili shuhudia mapigano ila kwa sasa hali imerudi tulivu .
Mkaazi alie hifadhi jina lake asema wanafunzi wali lazimisha Watoto wa shule kutoroka Shule zao na wengi hawakusoma kwani milio ya risasi ilishuhudiwa ,huku wanafunzi wengine wakitarajia kurudi shuleni baada ya tangazo la viongozi wa AFC/M23 ambao ndio wadhibiti Mji huo ulio achwa na serikali ya Kinshasa siku zilizo pita.
Mkuu wa Mkoa wa Kivu Kusini akiwa amewasili Bukavu baada ya kutangazwa rasmi na viongozi wa AFC Mjini Goma .huku akisubiriwa kuelezea wakaazi kwa njia ya radio ama ya TV kuhusu kilicho tokea Katika Mji wa Bukavu .wakaazi katika Mji wa Bukavu wakiomba wanao pigana kusitisha mapigano yao kwani wamechoshwa sasa na milio ya mara kwa mara eneo la mashariki mwa Congo DRC.