DRC

Wapinzani wa Rais wa sasa wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo waomba Felix Tshiskedi Felix kitisha mazungumuzo ya kisiasa kati yaw a Congomani kwa haraka kwani hali ni mbaya

JUNI 18, 2025
Border
news image

Akizungumuza na wafuasi wake katika hafla moja Mjini Kinshasa Marc Kabund alie kuwa mfuasi wake Felix Tshisekedi na kwa sasa akiwa upande wa upinzani baada ya kufungwa kwa muda mrefu katika gereza ya Makala kwa Zaidi yam waka mmoja kwa tuhuma ya kumuonea Rais amesema hali ya DR kwa sasa ni mbaya .

KaBund ameogeza kuwa Taifa la DRC lipo pa baya na watu wanao kuwa karibu na rais wamuambie kwamba " hali ni mbaya na huu si wakati wa kusikilivza wapiga ngoma na nyimbo za king'ora, wala kughairisha mambo, kwa sababu nchi yetu iko katika hatari ya kukandamizwa kuliko hapo awali. Tunamwambia kwamba yeye peke yake ndiye atakayebeba jukumu hilo mbele ya historia ikiwa jambo lisiloweza kurekebishwa litatokea kwa nchi yetu,"(( Jean-Marc Kabund.))

Kabundi amesema hayo wakati waasi wa AFC/M23 bado waendelea kudhibiti Mji wa Goma na Bukavu Kivu kaskazini na kusini ambako sehemu nyingine bado ipo mikoni mwa wapiganaji wazalendo na jeshi la serikali ya Congo.

MTV1 Online