DRC/DJUGU ITURI

Watu Zaidi ya ishirini wafariki Dunia kwa kuwawa kwa risasi na watu wanao dhaniwa kuwa CODECO

Julai 22, 2025
Border
news image

Baada ya wakaazi wa vijiji vya Lopa ,Nizi,Inga Bariere na solenyama ni miongoni mwa watu walio shuhudia uwepo wa wapiganaji wa CODECO wengi wao wakiwa Vijana wanao miliki silaha za risaisi ya Moto ambako wame vivamia vijiji vingi Tangu majuzi ,wakaiwa kati msako wa watu wanao dhaniwa kuwa wa CRP yake Thomas Lubanga.

Mkaazi mmoja wasema << Tume lazimika kukimbia na kuhama makaazi yetu kuona vijana wa silaha na wengine mapanga na tunajua hawa vijana hushambulia watu wasio kuwa na hatia ndio sababu mimi na majirani zangu wengine tumekimbia ,tunaomba serikali kuangalia haya mateso tunayo piitia kwani kwakweli tumeshindwa kuelewa nini hawa wappiganaji wanafanya huku katika uangalizi wa mkuu wa Mkoa ambae ni mwanajeshi.serikali lazima kutuambia nini tulifanya ili tuumie kwa mambo ambayo sisi wakaazi wa chini hatufahamu,tunauliwa kama wanyamapori,hata mnyama unakuta ni mzima kuliko mwana damu >>

Wasema wananchi mkoani Ituri ambako kumeshuhudiwa machafuko kwa muda mrefu bila mafanikio Zaidi katika usuluhishi.CODECO kwa upande wao wasema ,wako katika msako na doria za kuwatafuta wapiganaji wa CRP ambao ni wapiganaji wake Thomas Lubanga wanao taka kuchukuwa eneo la Ituri wakipinga serikali ya Kinshasa .

Ituri imekuwa ikishuhudia machafuko ikifatia mauaji na mashambulizi ya wakimbizi wa ndani ambao walipata hifadhi katika vijiji na miji yenye usalama ,baadae hushambuliiwa na watu wenye silaha.Serikali ikiomba watu wote wenye silaha kusalimisha silaha zao na kujiunga katika mchakato wa PDDRCS kwa ajili ya kurejeshwa katika maisha ya kawaida.

MTV1