DRC/LUBEERO MANGURUDJIPA

Watu zaidi ya sitini (60) wafariki Dunia kuUwawa na wengine kutekwa na watu wanao dhaniwa kuwa ADF katika kijiji cha Ntoyo kilometa nne na Mangurudjipa.

SEPTEMBA 09, 2025
Border
news image

Taarifa zasema watu hao walikuwa wakishiriki makesha ya mafariji.hadi sasa msako unaendelea kutafuta maiti zaidi.Akizungumuza na MTV ONLINE kiongozi wa shirika mpya la kiraia Etumba Babia anae kuwa na makao yake katika mji wa Mangurudjipa asema kwa sasa mili Zaidi ya sitini (60) imepatika baada ya watu wlaio kuwa kwenyee msiba kushambuliwa kinyama na watu wanao dhaniwa kuwa ADF.

Hadi sasa idadi kamili ikiwa haijulikane ,kwa saa za asubui mili ya watu abaini ilionekana na kwa sasa ikiongezeka baada ya msako katika mashamba ambako kulishuhudiwa mashambulizi ya wapiganaji hao.wengi walio kuwa kwenye msiba walikimbia mashambani na wengine wametekwa hatima yao ikiwa haijulikane hadi sasa

Mangurudjipa ni Mji unao patikana kwenye Zaidi ya kilometa miamoja magharibi mwa Mji wa Butembo kivu Kaskazini ambako wakaazi wa eeneo hilo wengi ni wakulima ,wachimba madini,wafugani ,wafanya biashara ambao wengi kwa sasa wameshindwa kujimudu kimaisha kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara.

Eneo hilo kukiwa kikosi cha jeshi tiifu kwa serikali FARDC na UPDF ya Uganda wanao kuwa eneo hilo katika msako wa ADF lakini bado ADF ikiendelea kushambulia wakaazi hasa wakulima na wana vijiji.

MTV1