Tanzania

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, amefafanua kuwa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025 - 2050 ina jumla ya shabaha 18, ambapo shabaha kuu ni kwa Tanzania kuwa na Pato la Taifa lenye thamani ya dola trilioni moja za Kimarekani na wastani wa pato la mtu mmoja lenye thamani ya dola elfu saba kwa mwaka ifikapo mwaka 2050.

Julai 17, 2025
Border
news image

Profesa Mkumbo ametoa maelezo hayo jijini Dodoma leo Julai 17,2025, wakati wa uzinduzi rasmi wa dira hiyo.

Pamoja na hayo , Profesa Mkumbo ameeleza kuwa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050 inalenga kuifikisha Tanzania kwenye uchumi wa juu unaotegemea maarifa, teknolojia na uvumbuzi

Naye Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameitaka Tume ya taifa ya mipango kuimarisha mifumo ya tathimini na ufuatiliaji ili kuhakikisha inazingatia mshikamano wa ngazi zote ikiwemo sekta za umma na binafsi

Tryphone Odace