TANZANIA

Ibaada Ya Elombe Yasaidia Kukuza Asali Na Tamaduni

DESEMBA 24, 2025
Border
news image

Wito umetolewa kwa jamii Mkoani Kigoma kuendelea kuwafundisha vijana mila, utamaduni na desturi za jamii husika kama njia ya kuchochea maendeleo na utu kwa jamii.

Hayo yameelezwa na Afisa maendeleo ya jamii Manispaa ya Kigoma Ujiji Aida Nzowa wakati wa ibaada ya kiasili ijulikanayo kama Elombe ambayo hufanyika mara moja kwa mwaka kwa kuwakutanisha watu kutoka maeneo mbalimbali duniani.

Amesema ibaada ya jadi na asili ambayo ipo chini ya shirika la maendeleo ya kijamii katika asili na tamaduni (SHIMKIATA) ni muhimu kuendelea kuenziwa kwani inasaidia jamii kurudi kwenye misingi ya upendo na mshikamano na kusaidia watu kutofanyiana mambo mabaya.

Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi, Mwakilishi wa kamati ya maandalizi ya ibada hiyo Muntu Bhabhantu amesema lengo lao ni kujenga jamii yenye mshikamo kupitia asili na tamaduni.

Kwa upande wake, Kiongozi wa wanajadi duniani Mwami Lokoko amesema jadi ina umuhimu katika kuwasaidia watu kutambua chimbuko lao na misingi ya kale.

Baadhi ya wananchi na viongozi wa kata ya Kitongoni walihudhuria ibada hiyo wamesema jamii kufundishwa jadi kupitia asili na tamaduni zao inasaidia kupunguza watu kufanya matendo maovu ikiwemo ukatili.

Ibaada hiyo imeenda sambamba na utoaji wa misaada kwa wasiojiweza, kufungisha ndoa mbili za kimila ikiwa chini ya kaulimbiu isemayo “Elombe ni urithi wetu, Amani yetu, Umoja wetu, Faraja kwa wenzetu kwa maendeleo endelevu.”

MTV1 Online