Juma tatu tarehe kumi na tisa elfu mbili ishirini na tano walio rudishwa kwao katika usaidia wa UNHCR ikuwa 789 wengi wao wanawake ila kukiwa vile wazee, watoto na vijana wachache. Juma mosi watu 300 walirudishwa Rwanda kutoka DRC kupitia Mji wa Goma. Kwa jumla, watu ambao wamerudishwa Rwanda kutoka Vijiji vya Masisi na Nyiragongo na wengine katika Mji wa Goma ikiwa 2089, wasema M23.
Baadhi yao wasema kwamba walikuwa wakiambiwa na wazazi wao kwamba walitokea katika taifa la Rwanda wakati wa vita vikali, na kwa sasa walikuwa tayari wameshapata mashamba katika misitu na mikoa mashariki mwa Congo ambako walikuwa wameunda familia. Wengi walikuwa na miaka mitatu, wengine miwili, wengine tano, yaani wakati walipo kimbia na wazazi wao ambao wengi wameshafariki dunia.
Walipoingia Mjini Gisenyi Rwanda wasema hii ni mara ya kwanza kuingia Rwanda kwani walikuwa wakiambiwa tu kwamba kwao ni Rwanda, ila wanafurahi kurudi nyumbani kwao. Walikuwa wanaambiwa na wapiganaji wa FDLR kwamba wasirudi nyumbani kwao kwani watauwawa na serikali ya Rwanda.
Mea wa Rubavu Rwanda anasema watu hawa wote wanapelekwa katika center ya mpito ambapo watafanya wiki moja kwa ajili ya kukaguliwa na kuulizwa vijiji vyao. Baadaye, watapelekwa katika center za kuwarudisha katika maisha ya kawaida na wengine katika vijiji vyao ama kuishi katika taifa wanazotaka.
Lakini hata hivyo, kati kati yao kuna raia wa Congo DRC ambao ni wanawake walio olewa na hao wakimbizi wa Rwanda, wengine wakiwa katika kundi la FDLR kwa sasa na makundi mengine yanayo kuwa katika mbuga la Virunga. Mchakato huu ni mrefu sana ambao unawalenga kwa jumla watu kutoka Kabila la Wahutu.
Mama mmoja tuliyozungumza naye akiingizwa katika basi asema yeye si raia wa Rwanda na amewaacha watoto wake tano, kwa hiyo anahitaji arudishwe kwao DRC kwani yeye aliolewa na mwanaume kutoka kabila la Wahutu, ila yeye kwao sio Rwanda. Lazima UNHCR imsaidie kurudi nyumbani kwao DRC.