Takriban wapiga kura 132 wa makadinali, wenye umri wa chini ya miaka 80, watakusanyika nje ya milango iliyofungwa katika Kanisa la Sistine Chapel kumchagua papa mpya, siku kumi na saba baada ya kifo cha Papa Francis.
Siku ya Jumanne, siku moja kabla ya kuanza kwa kongamano hilo, Chuo cha Makardinali kilikazia sifa muhimu kwa Papa wa baadaye, anayepaswa kumwilisha sura ya mchungaji mwema, mchungaji wa Kanisa la Wasamaria.
Kwa jumla, makadinali 173, wakiwemo wapiga kura wa makadinali 130, walishiriki katika mkutano mkuu wa kumi na mbili, anaeleza Matteo Bruni, mkurugenzi wa Holy See Press Office.
Baadhi ya wa kristu kutoka Africa wakiomba Baba mtakatifu kutoka Africa kwani mataifa ya wazungu umeongoza kanisa kwa muda mrefu na wengi wao wakianza kupoteza mila za kibinaadamu.