DRC/KIRUMBA

Kundi la waasi wa M23 laweka viongozi wapya wa Mji wa Kirumba wilayani Lubero Kivu Kaskazini mashariki mwa Congo DRC baada ya walio kuwa kupewa nyazifa nyingine

APRILI 23, 2025
Border
news image

Wakaazi wa Mji wa Kirumba wameandamana na kutembea kilometa mbili kwa miguu wakishinikiza viongozi hao wapya ambao wanakabidhiwa uongozi wa Mji wa Kirumba na miji mingine ainayo kuwa chini ya uongozi wa waasi hao wa M23.

Wilayani ya Lubero sehemu kubwa na muhimu kwa sasa ikiwa katika mikono ya M23 na sehemu ndogo ikiwa mikononi mwa serikali ya Kinshasa, huku wasiwasi ikianza kutokana na mazungumuzo ya Doha kusuasua.

Waasi wa M23 walichukuwa hii juma nne vijiji vya Bunyatenge baada ya Mbughavinywa, vijiji vilivyo kuwa mikononi mwa wapiganaji wazalendo wali fukuzwa wiki ilio pita, hii baada ya kundi la FPP/AP lake Kabido kuwagawanyika kwa vipande tafauti.

AM/MTV News DRC