Baadhi ya waandamanaji nchini Tanzania waomba vyombo vya ulinzi na usalama kudhibiti hali ya usalama kwa ajili ya usalama wa taifa. Hii kufuatia maandamano ya siku tatu ambayo yamesababisha uharibifu na uporaji wa mali na vitu vya watu binafsi pamoja na vituo vya polisi.
Hii ikiwa siku ya tatu ya maandamano tangu ulipofanyika uchaguzi nchini Tanzania, Tume Huru ya Uchaguzi Zanzibar imetangaza mshindi wa kiti cha urais HUSSEIN MWENYI kwa upande wa Zanzibar.
Eneo kubwa akiendelea kuongoza SAMIA SULUHU. Wananchi wanakosoa Tume Huru ya Uchaguzi kwa kuwatenga viongozi wakuu waliowekwa kando katika kinyang’anyiro hicho cha uchaguzi, ambao waandamanaji wanaomba ufutwe.
Hii ni mara ya kwanza tukio kama hili kutokea Tanzania katika historia, wananchi wakiandamana na kuzua vurugu, kwani Tanzania imekuwa taifa la mfano wa amani Afrika Mashariki.