DRC

Mahakama ya kijeshi Wilayani Lubero yatangaza hukumu kwa askari tiifu kwa Serikali

FEBRUARI 06, 2026
Border
news image

Mahakama ya kijeshi ya tangaza hukumu ya kifungo cha maisha kwa askari mmoja wa serikali baada kukutwa na makosa ya mauaji na ubakaji.

Likasu Zuzu Ngombi askari jeshi wa brigade ya 21 amehukumiwa kifungo cha maisha baada ya kukutwa na makosa ya ubakaji ya mama mkulima eneo la Mangurudjipa secta ya Bapere wilayani Lubero.

Mahakama ha kijeshi ilianzisha dhidi ya wanajeshi walio shutuliwa na kukamatwa na vyombo vya usalama eneo la Mangurudjipa wilayani Lubero baada ya malalamiko ya wakaazi wakilaumu vitendo vya wanajeshi.

Pamoja na hayo eneo hilo lili shuhudia uporaji, mauaji pamoja na ubakaji. Mmoja wa waathirika akiwa Kisuba Jacqueline wa umri wa miaka arubaini na saba aliyeuawa katika shamba lake la N. Tembe magharibi mwa Mji wa Mangurudjipa.

Mahakama ya kijeshi eneo hilo ilisema hii itakuwa funzo kwa watu wengine wanaokuwa na silaha wakiwemo askari jeshi tiifu kwa serikali na wazalendo ambao washutumiwa na wakaazi, yasema mashirika ya kiraia.

Secta ya Bapere ni miongoni mwa maeneo yanayoshuhudia visa vya mauaji kutoka kwa watu wenye silaha wanaodhaniwa kuwa ADF na watu wengine ambao bado uchunguzi unaendelea.

Ripoti kutoka mashirika yasiyo ya kiraia zasema watu zaidi ya elfu mbili mia sita arubaini na tano (2,645) wameuawa katika eneo la Bapere na Baswagha tangu mwaka elfu mbili ishirini na nne katika uangalizi wa serikali na Umoja wa Mataifa kupitia MONUSCO.

MTV1 Online