DRC - LUBERO

Mashirika yasiyo ya kiserikali Butembo yaishinikiza Serikali ya Kinshasa kuchukua hatua za haraka kuboresha hali duni ya wafungwa katika Gereza Kuu la Kakwangura, Kivu Kaskazini

JANUARI 06, 2026
Border
news image

Mashirika yasiyo ya kiserekali Katika mji wa Butembo kivu Kaskazini mashariki mwa Congo waomba serikali ya Kinshasa kupata suluhisho kuhusu hali mbaya wanayo pitia wafungwa katika gereza kuu ya kakwangura Mjini Buteembo.

Katika ripoti ya mwisho wa mwaka wa elfu mbili ishirini na tano (2025) shiria la prime métal mundu ngawe, ikiwa ni shirika lisilo la kiserekali Katika Mji wa Butembo, lapongeza hatua ya vyombo vya sheria vya DRC kuanzisha mchakato wa kupunguza wafungwa katika gereza mbali mbali, wengi wao wakibaki gerezani bila kufikishwa mahakamani ama kusikilizwa.

Shirika hilo lasema Gereza ya Kakwangura Mjini Butembo kwa sasa inashuhudia hali ngumu kwa wafungwa ambao ni wengi kuliko idadi kamili, kwa sasa kukiwa wafungwa 1300 ambao bado wasubiri hatua ya serikali ya Congo DRC kuwaachilia wafungwa ambao wengi wako katika hali mbaya. Wengi wao wakiwa na makosa ambayo sio ya kutisha, hasa wanawake.

Hata hivyo shirika hilo limeomba serikali pamoja na Umoja wa Mataifa kupitia MONUSCO kulipa deni za tiba kwa wafungwa waliotibiwa katika hospitali ya Kitatumba, wakiwa na deni ya dola zaidi ya elfu mbili. Utafahamu kwamba katika baadhi ya gereza nyingi wafungwa hushughulikiwa na watu binafsi hasa kutoka kwa makanisa wanaochangia vyakula kusaidia wafungwa.

Wafungwa wengi huambukizwa na maradhi kutokana na harufu mbaya inayotokana na ukosefu wa usafi gerezani. Utafahamu kwamba wafungwa zaidi ya elfu moja mia tatu (1300) wahifadhiwa kwenye gereza la Kakwangura mjini Butembo, wengi wao wakiwa bado hawajafunguliwa kesi ama kuelezewa kwanini walifungwa.

Abel Tsongo - MTV1 Online