Watu wasio pungua tano wauwawa wakati wa shambulizi la watu wanao dhaniwa kuwa ADF katika kijiji Mangandu kipatikanacho karibu na Mji wa mbau wilayani Beni kivu kaskazini.
Hali ya wasiwasi yazidi kushuhudiwa katika vijiji mbali mbali wilayani Beni kufatia shambulizi na mauaji ya watu inaendelea kushuhudiwa katika baadhi ya maeneo ya wilaya ya Beni hasa wakulima ambao washambuliwa wakiwa mashambani .
Watu zaidi ya tano wameuwawa hii juma tano kumi na mmoja kwenye mashamba inayo unganisha Mbau Mantumbi baada ya kuviarifu vyombo vya usalama bila mafanikio.
Wakaazi Wa Beni washutumu uzembe mkubwa katika vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo vya pewa taarifa na badae watu kuwawa.
Vijiji vinavyo patikana barabara MBAU-MANTUMBI vikiwa miongoni mwa vile ambavyo vimeshuhudia mashambulizi na watu kuwawa na wengine kutekwa hadi porini katika uangalizi wa serikali na umoja wa mataifa kupitia MONUSCO.
Vijana wa lucha katika Mji wa Beni wameomba serikali kuu ya Kinshasa kufuta na kuondoa kwa haraka uongozi wa kijeshi (État de siège) ambayo haifai kwa wananchi kwani wakaazi bado waendelea kuwawa katika uangalizi wa viongozi.
kiongozi wa shirika la kiraia katika secta BENI - MBAU aomba wakaazi kuwa waangalifu na viongozi kuwajibika.