Hii ni baada ya mapigano makali yaliyo ilio shuhudiwa kati ya kundi la Wapiganaji wazalendo wa kikundi cha Bana balamuka dhidi Ya ngome ya waasi wa AFC/M23 pa Kamandi gîte asubui mapema leo saa kumi na nusu za alfajiri 21 April 2025. Duru za kiraia Kutoka eneo hili za repoti kwamba wazalendo hao walitokelea ndani ya bonde la mbuga la wanyama la Virunga pembeni ya ziwa Édouard na kutwangana na AFC/M23 katika Kijiji cha Kamandi gîte.
Taarifa za sasa zasema huenda watu wa tatu wamefariki Dunia kwa kuuwawa na vipande vya Bomu ilio angakukia mkaazi ya watu. Waasi wa AFC/M23 watangaza kuwapa pigo wapiganaji wazalendo na kwa sasa hali ikiwa imerudi Tulivu wapiganaji hao wengi wao wakiwa Vijana wakiwa wametoroka na kurudi katika mbuga la Wanyama pori la Virunga.
Mapiganao ambayo yana jiri baada ya baadhi ya wazalendo kupuuza mwito wake Willy Mishiki kutoka wazalendo anae kuwa na makao yake Mjini Kinshasa.