Katembo Mukosa John kutoka Kijiji cha kyanganda katika eneo la baswagha alifariki Dunia baada ya kufunikiwa na matope yenye mawe wakati wa mporomoko wa mgodi jumatatu 2 juny wakati aliokuwa akichimba madini .Tukio kama hizi hutokea mara kwa mara katika migodo mbali bila watu kufahamu ,wenye migodi wakiogopa kusema ukweli .
Musubaho kamanda wa polisi inayohusika na uchunguzi madini eneo la Manguredjipa katika secta la Bapere,Mukosa mwenye umri wa miaka Zaidi ya arbaini alifariki kwa kuangukiwa kwa kwa matope yenye mawe eneo la uchimbaji wa madini la pangoy linalo ongoza na shirika la Mahoho coopérative Mining(Macomin).baada ya uchunguzi mwili wa Mukosa John ulikabidhiwa kwa familia na kuzikwa baadae.
Mumomonyoko wa ardhi katika eneo za uchimbaji madini imekua ikijitokeza mara kadhaa hii ikiwa changamoto kwa wachimbazi wanao tumia mikono kwa kuchimba madini ambayo hata hawafaidiki na familia zao zikipitia maisha magumu .Watu wengi wanao chimba madini ni kutoka vijiji na miji ya mbali kujaribu kujikimu kimaisha ,eneo la Maangurudjipa likishudia mashambulizi ya mara kwa mara kutoka watu wanao dhaniwa kuwa ADF.
Mwishoni mwaka wa elfu mbili ishirini na nne (2024) zaidi tano walifariki Dunia kutokana na mmonyoko wa ardhi eneo la uchimbaji madini la Pangoy na Makwasa Manguredjipa Lubero ,visa vizivyo ripotiwa mara kwa mara..