Taarifa zasema jioni ya Februari 4, 2026, wakaazi wa Salamabile walikubwa na bumbuazi kutokana na janga kubwa na msiba kwa wakazi wa Barabara Dominique, iliyoko katika kitongoji cha Namoya katika wilaya ya mashambani ya Salamabila, eneo la Kabambare.
Moto ambao bado haujajulikana asili yake uliteketeza zaidi ya nyumba 16, na kuacha takriban familia 21 bila makazi wakiwemo wanawake na watoto.
Kulingana na tathmini iliyofanywa na wafanyikazi wa IFAPPDE waliokuwepo uwanjani, wasema watoto miamoja na tano (105) walipoteza vifaa vyao vya shule, na vitu kadhaa vya thamani viliharibiwa kabisa na moto ambao chanzo chake hakijajulikana.
Hali hii huwaweka wanawake na watoto katika hatari kubwa za ulinzi, hasa kwa vile familia zilizoathiriwa hulazimika kutumia usiku wao nje, bila makazi au usaidizi wa kutosha. Kutokana na maafa haya, IFAPPDE inatoa wito wa dharura kwa mamlaka za mkoa na washirika wa kibinadamu kuingilia kati mara moja kuokoa maisha na kufanya tathmini ya haraka ya mahitaji ya kaya zilizoathirika.
Kwa IFAPPDE–Maniema