DRC
Raia wa Kabila la wabatwa ama wambuti waomba kushirikishwa katika mchakato wa amani na usalama
JUNI 05, 2025
Wambuti nchini DRC waomba serikali ya Kinshasa yake Felix Tshisekedi kuwashirikisha katika michakato mbali mbali ya amani na usalama pamoja na maendeleo nchini DRC.
Mboni Samuel ni mmoja wa Wambuti Kivu Kaskazini ambaye ametembelea Vuyinga, kijiji cha Vumbuti, ambako raia hao wanapitia hali mbaya na ngumu ya kimaisha. Wengi wao wakiwa hawana vyakula, mavazi, dawa hospitali, shule, wakilalamikia ukosefu wa usalama hasa wakishutumu watu wenye silaha kuwachapa fimbo.
Desire Mungusa ni mmoja wa wazee wam...