Katika siku ya pili ya ziara yake katika jimbo la Lualaba, Rais Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo alifungua Mkutano wa 12 wa Magavana wa Mikoa Jumanne hii kwenye makao ya Congress mkoani Kolwezi.
Mfumo wa mashauriano ya mara kwa mara kati ya majimbo na serikali kuu ya kitaifa, Mkutano wa Magavana unaleta pamoja magavana na manaibu wao wa majimbo 26, marais wa Mabaraza ya Mikoa, mawaziri wa kisekta, na wataalam kutoka taasisi, wakiongozwa na Rais wa Taifa.
Wakaazi wa Mkoa wa Lualaba wakiomba mikutana kama hii kufanyika mara kwa mara ili uongozi uwe karibu na wananchi na mawaziri ama wakuu wa taifa kufahamu matatizo wanayopitia wananchi wa chini.
Wakaazi wa mashariki wakikemea utawala ambao unagubikwa na wizi wa pesa za serikali na kuomba Félix Tshisekedi kuwaadhibu wafanyakazi wa serikali wanaoiba pesa za serikali na kutumia rushwa kwa uharibifu wa taifa ambalo tangu ukoloni bado halina maendeleo nyati.