Baada ya Muda mrefu na taifa la Congo likiendelea kupitia msuko suko wa kisiasa na kiusalama Rais wa Congo Feleix Tshisekedi na mwanasiasa alie shindwa uchaguzi Martin fayulu wamekutana hii Alhamisi, Juni 5, 2025 katika ukumbi wa Palais de la Nation Mjini Kinshasa.
kiongozi wa upinzani Martin Fayulu alithibitisha nia yake ya kuunda "Kambi ya Nchi ambayo inaweza unganisha wanasiasa wote kwa ajili ya kupambana na uvamizi ."
Fayulu anasema lazima wanasiasa wote kuweka nguvu na kuwaleta pamoja wahusika wa kisiasa wa Kongo kushughulikia mzozo wa usalama unaokumba eneo la mashariki mwa nchi hiyo:
"Ilikuwa rahisi sana. Unajua kwamba taifa letu linapitia kipindi kigumu sana. Tunashambuliwa kutoka kila mahali, tunahitaji uwiano wa kitaifa. Nilikuja kumwambia (maelezo ya Mhariri: Rais Tshisekedi) kwamba hatuna suluhu 36: lazima tuunde kamati ya pamoja itakayo unganisha watu wote wanao penda taifa wanaopigania nchi yao."
Kwa rais wa chama cha Citizen Engagement for Development (ECIDé), "migogoro hii yote tunayopitia-usalama, kijamii, kisiasa-yana suluhisho moja tu: mazungumzo kati ya wa Congomani kukaa kwenye meza moja ."
Martin Fayulu pia alimhimiza Félix Tshisekedi kuzungumuza na wakuu wa kanisa hasa maaskofu wa CENCO na wachungaji wa ECC, ili kuangazia mapatano yao ya kijamii ya amani na kuishi pamoja vizuri.
Baadhi ya wanasiasa wamesha kimbia mji wa Kinshasa yaani DRC nakuwa wakimbizi katika mataifa mengi katika kile wanacho sema udicteta unao anza nchini DRC japo taifa hilo limesha kubali kuweka Udemokrasia.