DRC

Serikali ya Kinshasa na waasi wa AFC/M23 wageuka washirika wa amani na usalama

APRILI 25, 2025
Border
news image

Baada ya kukutana Doha, Qatar, serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waasi wa M23/AFC wakubaliana kwa sasa kuingia katika mchakato wa kutafuta amani na usalama mashariki mwa Congo na Maziwa Makuu, ambako kumeshuhudiwa mapigano kwa muda mrefu, mapigano yaliyo sababisha watu kuhama makaazi yao na kuwa wakimbizi wa ndani.

Serikali ya DRC na waasi wa M23 wameomba kanisa, vyombo vya habari, na wadau wengine kushinikiza mchakato huu muhimu wa kutafuta amani na usalama kwa ajili ya kuokoa maisha ya maelfu ya watu wanaoendelea kutaabishwa na machafuko ya muda mrefu mashariki mwa Congo.

Siku zilizo pita, serikali ya Kinshasa ilikuwa ikiwaita waasi wa M23 kuwa magaidi, lakini kwa sasa maneno kama hayo yamepigwa marufuku, na vitisho dhidi ya watu kuwashota vidole kuwa ni waasi wa M23 vimesitishwa. Miongoni mwa mapendekezo ya waasi ni pamoja na kuwaachilia watu wote waliofungwa kutokana na uasi wa AFC/M23 pamoja na kurudisha mali ya watu iliyochukuliwa na serikali ya Kinshasa.

Mazungumzo hayo yanajiri baada ya Rais wa Rwanda na wa Congo kukutana Doha, huku Marekani na mataifa mengine yakiomba mataifa hayo kujenga umoja kwani ni majirani. Rwanda inatakiwa kuondoa wanajeshi wake nchini DRC, pamoja na DRC kuwasaka wapiganaji wa FDLR ambao ndio chanzo cha mzozo wa muda mrefu mashariki mwa taifa hilo tajiri Afrika Mashariki, Maziwa Makuu, na Afrika ya Kati na Kusini.

Kwa sasa waasi wa M23 wakiwa wameshachukua sehemu kubwa ya Kivu Kaskazini na Kusini. Wakimbizi wa ndani wameshaanza kurudi kwenye vijiji vyao baada ya waasi wa AFC/M23 kuchukua miji ya Goma na Bukavu.

AM/MTV News DRC