DRC
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia Wakimbizi limesema zaidi ya raia wa Kongo 50 waliokimbia vita mashariki mwa nchi yao wamekufa nchini Burundi
JANUARI 11, 2026
Shirika hilo limesema kati ya jumla ya vifo 53 vilivyorekodiwa, watu 25 wamekufa kutokana na mlipuko wa kipindupindu, huku wengine sita wakifariki kutokana na upungufu wa damu na matatizo mengine yanayohusiana na utapiamlo.
Jean Jacques Purusi, gavana wa jimbo la Kivu Kusini ambapo Uvira iko, ameieleza hali inayowakabili raia wa Kongo waliokimbilia Burundi kuwa ni ya "taabu" na kwamba ni mgogoro uliosahaulika na jamii ya kimataifa.
Burundi kwa upande wake haijatoa maoni juu ya taarifa hiyo.