DRC

Spika was Bunge nchini Congo Aimé Boji aomba wakaazi wa Beni kushikamana na kujenga Umoja

FEBRUARI 20, 2026
Border
news image

Boji ameomba raia kuweka kando ukabila na kuunga mkono juhudi za jeshi la Congo kwani hakuna jeshi bila wananchi.

Aimé Boji amesema hayo akiwa Mjini Beni ambako atarajia kukutana na kundi mbali mbali za watu, pamoja na hayo Boji ameomba wananchi wa DRC kuunga mkono mchakato wa Marekani na Doha kwani ndio peke kwa ajili ya amani na usalama mashariki mwa Congo.

Spika wa Bunge la Congo amefika Beni vijiji vingi vikishuhudia mashambulizi ya watu wanao dhaniwa kuwa ADF kushambulia watu wilayani Beni na Lubero pamoja na sehemu moja mkoani Ituri.

Vijiji vingi kwasasa vikiwa vimesha ota majani na makaazi ya watu kuota miti na mimea kuharibika mashambani.

Mauaji na mashambulizi ikitekelezwa katika uangalizi wa serikali na umoja wa Mataifa kupitia MONUSCO ambao wana askari wengi Mjini Beni na vifaa muhimu vya kijeshi.

MTV1 Online