DRC

Viongozi wa M23 katika Mji wa Kirumba wilayani Lubero Kivu Kaskazini mashariki mwa Congo DRC wafanya kambeni kuhusu usalama Katika Mji wa Kirumba kusini mwa Lubero

MEI 20, 2025
Border
news image

Hamasa kubwa imefanyika na viongozi hao katika kata mbali mbali za Mji wa Kirumba wakaazi wakiombwa kutaja sehemu wapatikana watu wenye silaha na majambazi, Munyandekwe Fizi Innocent ameomba wakaaji wa muji wa Kirumba kuwa na umoja kati yao na kuepuka ubaguzi wa kikabila, na kujenga ushirikina bora.

Munyandekwe Fizi ameomba vijana wenye nguvu kujiunga na uasi wa AFC/M23 kwa ajili ya kulinda na kuweka usalama katika vijiji vyao na wakulima kuendelea na majukumu yao ya kilimo, mbali na jeshi wakaazi wakiombwa kuingia katika polisi ambayo italinda usalama wa wakaazi, kata Makasi ikiwa mmoja wapo wa kata zilizo lengwa moja kwa moja.

Kirumba eneo eneo muhimu kwa wilaya ya Lubero ambako siku zilizo pita kulishuhudiwa mapigano makali kati ya jeshi la Congo FARD wakiungana na wazalendo dhidi ya M23, mashamba na vijiji vikishuhudia tatizo za vifaa vya kijeshi hasa bomu ndogo ndogo zinazo tatiza wakulima.

Wakaazi kwa upande wao wakiomba suluhu la haraka kati ya serikali na M23 kupatikana kwani wao kwa sasa wapitia hali ngumu na mbaya ya kimaisha na ukosefu wa usalama katika baahi ya Miji ikiwemo Goma na Bukavu ambako watu huingiliwa kila siku.

MTV1 Online