DRC

Waasi wa AFC /M23 waondoa askari wao katika mji wa katondi wilayani Lubero

APRILI 02, 2026
Border
news image

Katondi ni eneo ambalo lipo kilometa kumi na nane kutoka Mji wa Lubero, mji mkuu wa wilaya ya Lubero Kivu Kaskazini mashariki mwa DRCongo. Eneo hili lilikuwa ngome muhimu kwa askari wa ARC ambao ni askari jeshi wa M23, waliokuwa mstari wa mbele wa mapigano.

Kuondoka kwa M23 katika Mji wa Katondi ulio karibu na Mji wa Kitsumbiro ni mfululizo wa hatua kadhaa zilizochukuliwa wakati wa makubaliano kati ya serikali ya Rwanda na DRC chini ya usuluhishi wa serikali ya Marekani kwa kumaliza mzozo wa mashariki mwa taifa la Congo DRC.

Eneo hili la Katondi likiingia katika orodha ya maeneo mengine mengi yaliyoachwa na AFC-M23 Kivu Kaskazini hasa Masisi, Lubero na Walikale, ni kama njia ya kupisha mazungumzo kwa pande mbili kwa kumaliza mzozo wa mashariki mwa taifa hili na maziwa makuu.

Kulingana na makubaliano, pande zote zinapaswa kurudi nyuma kila mmoja kilometa tano au zaidi ili kuepuka mapigano na maeneo hayo yakabidhiwe kwa Umoja wa Mataifa kupitia MONUSCO. Hata hivyo, hili ni gumu kutekeleza kwani kwa sasa maeneo mengi yamedhibitiwa na serikali na wazalendo ambao wanasema ni kurejesha utawala wa serikali tawala.

MTV1 Online