DRC

Waasi wa AFC-M23 waondoa askari wao kwenye musatari wa mbele wa mapigano wilayani lubero kivu kaskazini

MACHI 30, 2026
Border
news image

Wakaazi wa vijiji vya Kipese, Katondi, Kitsumbiro, Vunyakondomia, Luvango na vijiji vingine wameshuhudia milolongo ya askari wa M23 wakirudi na mizigo na vifaa vya kijeshi eneo la Ndoluma wakielekea Alimbongo wakitembea kwa miguu na kuacha ngome zao ambazo walidhibiti siku kadhaa zilizopita. Hadi sasa hakuna ujumbe wowote wa M23 na wakaazi wakiwa na mshangao mkubwa.

Kuondoka kwa askari wa M23 katika miji muhimu wilayani Lubero kunaweza kudhoofisha chama hicho na kupoteza wafuasi wengi walio kuwa wamejiunga kutoka vijiji mbali mbali vya Lubero na sehemu nyingine waliotegemea kwamba chama hicho kitaweza kuendelea ama kusonga mbele.

Marekani kwa sasa imekuwa ikiweka shinikizo kwa serikali za Rwanda na DRC kuheshimu makubaliano walioafikiana siku zilizopita kwa ajili ya amani na usalama mashariki mwa taifa la Congo DRC na kumaliza tatizo la wapiganaji wa FDLR ambao wamekuwa chanzo cha mzozo wa mara kwa mara.

FDLR imeripotiwa kwa muda mrefu katika mbuga la wanyama pori la Virunga kwa zaidi ya miaka thelathini, wakishutumiwa katika uharibifu wa mazingira na uwindaji haramu wa wanyama pori.

MTV1 Online