DRC

Wailslam nchini Goma waungana na wenzio kusherekea Eid kuu hii ikiwa muhimu zaidi kwa Dini yao

JUNI 05, 2025
Border
news image

Akizungumuza na MTV1 ONLINE AL -Katanti asema siku hii ni muhimu katika mila na desturi ya kiislam kwa kila familia hu chinza mnyama wa miguu nne ,Mbuzi ,Kindo ,Ngombe kama halama na matoleo kwa mwenyezi Mungu .

Wazee ,watu wazima,vijana ,wanawake na watoto leo walijitokeza katika barabara kuu na ndogo Mjini Goma Mji ambao unadhibitiwa na uasi waa AFC/M23 ,hii ikiwa mara ya pili kufanyika katika Mji wa Goma tangu Mji huu uwe mikono mwa waasi.

Laurence Kanyuka msemaji wa AFC/M23 ameomba waislam wote kuchangia amani ,maridhiano na Umoja hasa wakishawishi vijana wenye silaha kurudisha silaha hizo kwa uongozi wao kwani ziliachwa na wanajeshi wa Kinshasa walipo kimbia mji wa kuondoka zao kwa sasa silaha hizo zikiwa tishio kwa usalama wa wananchi.

Mea wa Mji wa Goma Julien Katembo kwa upande wake apongeza waislam kujenga umoja na kusameheana kwa yote yalio pita na kusali pamoja kwa ajili ya amani wakisubiri viongozi wapya siku zijazo .

Sherehe za leo zimeafanyika katika ulinzi mkali wa askari wa ARC yaani wa waasi wa M23 ambao waliweka ulinzi mkali kote Mjini na ukaguzi wa makini.

Waislam kwa upande wao wakisema muda ndio huu wa Congo kupata amani na usalama na wanasiasa wote kuhakikisha wanamaliza matatizo uao kwa njia ya mazungumuzo.

MTV1 Online