DRC /OICHA /BENI

Wakaazi wa vijiji mbali mbali wilayani Beni Kivu Kaskazini waomba serikali kuchukuwa hatua kuhusu usalama wao

SEPTEMBA 10, 2025
Border
news image

Baada ya mashambulizi na mauaji ya watu katika eneo la Fotodu magharibi mwa mji wa Oicha wilayani Beni, wakaazi na wana harakati wakerwa na msimamo wa serikali ya Congo DRC kufatiaa ukimia wake dhidi ya mauaji ya wakaazi wa Beni na Lubero na sehemu moja ya Ituri.

Hii baada ya ya watu kumi na nane mili yao kuppatikana wakiwa wameuwawa, miongoni mwao wanawake wa tatu (3) na wanaume kumi na tano (15) wote wakiwa wakulima walio kuwa wakilima shamba zao hii juma nne tisa septamba elfu mbili ishirini na tano.

Mauaji ambayo yanatekelezwa na watu wanao dhaniwa kuwa ADF ambao kwa zaidi ya miaka kumi na tano sasa waendelea na mauaji katika uangalizi wa Vikosi vya Umoja wa matifa kupitia MONUSCO ambao wana askari wengi na silaha nzito, pamoja na jeshi la serikali ya Congo FARDC ambalo limedhidiwa na mauaji hayo ambayo imesababisha vifo vya watu wengi zaidi.

Mauaji haya yana jiri pamoja na mengine ilio tokea siku moja yaani juma nne katika kijiji cha Ntoyo kilometa chacha na Mji wa Mangurudjipa.

Mkaazzi mmojana mkulima hapa asema:

((Wapendwa wenzangu,

Hivi sasa, ADF inatembea ikwa uhuru katika maeneo kadhaa: Fotodu, Mavete, Kukutama, Pwendi, Kithevya, Manzanzaba, Aveyi, Maleki, Kasopo, Mulolya, Musuku. Idadi kubwa ya watu waishi katika uhoga na ukosefu wa usalama kabisa, wakati mamlaka kuu ya mkoa wanaonekana kuukaa kimia japo uongozi wa mkoa uko Beni.

Hatuwezi kuendelea kukabiliwa na vifo kila siku wakati tupo katika serikali ya kutumia nguvu, hatujaelewa kwanini serikali ya mkoa inayo ongozwa na jeshi wameshindwa tulinda sisi wakaazi kama wameshindwa waseme basi tujilinde. Hatujaona majibu sabiti kwa mahitaji na usalama wetu.

Hii inaonekana kuwa viongozi wana fahamu haya mauaji ndio sababu wakaa kimia, hata Rais hawezi toa pole kwa wananachi wake. Mbona mataifa mengine hata watu kumi wakifa Rais anasimama, hii ya Beni na Lubero ni jama ama kuna nini, anasema mkaazi na mkulima mmoja wa Beni.))

Kwa mda mrefu sasa watu waendelea kuwawa na vijiji kuchomwa moto na watu wanao dhaniwa kuwa ADF chini ya uangalizi wa serikali na vyombo vya usalaama pamoja na Umoja wa Mataifa ukikaa kimia wakishughulikia swala la uasi wa AFC/M23.

MTV1 Online