Wakakazi wa Vijiji vya Lunyasenge wilayani Lubero walazimika kuhama na kukimbia vijiji vyao kufatia mapigano makali kati ya M23 na wapiganaji wazalendo.
Wakiwa na hofu, idaidi kubwa ya wakaazi wa Lunyasenge wa wasili katika Mji wa Kyavinyonge unaopatikana wilayani Beni pembezoni mwa ziwa Édouard Kivu kaskazini mashariki mwa DRC. Hii ni baada ya Kijiji jirani cha Lunyasenge Lac kilichopo wilayani Lubero pembeni ya ziwa Édouard kuzibitiwa Ijumaa mbili Mei elfu mbili ishirini na tano.
Waasi wa AFC/M23 wakiwa wamechukua Kijiji cha Lunyasenge karibu na Kyavinyonge na kusababisha hofu kubwa miongoni mwa wakaazi wanaohofia mapigano makali kutokea kwa mara nyingine kati ya waasi hao na wapiganaji wazalendo. Taarifa zinasema wakaazi hao walio kimbia makaazi yao wametumia boti ndogondogo na wengine wakitembea kwa miguu safari ndefu, wakiwemo watoto na wazee wakibeba vitu vyao.
Wakaazi hao wakikimbilia eneo lenye usalama zaidi, utaona kwamba tangu wiki mbili sasa eneo hilo limekuwa likishuhudia mapigano kati ya wazalendo na M23 katika vijiji vya Kamandi Lac, Kisekera, Taliha, na Lunyasenge pembezoni mwa ziwa hilo.
Mapigano yanayo jiri wakati serikali na waasi wapo kwenye mazungumzo Doha, Qatar na wengine Marekani, hasa Rwanda na DRC, kuhusu ushirikiano kati ya mataifa mawili ambayo kwa sasa yako kwenye uhusiano mbaya tangu vita vya M23, japo mataifa hayo mawili yako katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
M23 imekuwa ikisema itaendelea na mapigano hadi miji ya Kisangani na Kinshasa hadi pale watakubaliana pamoja. Laurence Kanyuka, msemaji wa AFC/M23, alisema mazungumzo kati yao na serikali hayawezi kuwazuia kujilinda na kusonga mbele kuchukua eneo, kwani hawana imani na serikali ya Kinshasa isiyo heshimu makubaliano.