DRC

Wasiwasi umekumba Mangurudjipa, Lubero, Kivu Kaskazini, baada ya shambulio la watu wenye silaha katika kata ya Mambembe, kilomita 70 magharibi mwa Butembo

news image

Hali ya wasiwasi yaripotiwa Katika Mji mdogo wa Mangurudjipa wilayani Lubero Kivu Kaskazini baada ya watu wenye silaha kushambulia kata Mambembe katika Mji huo Mdogo unao patikana Zaidi ya kilometa sabini magharibi mwa Mji waa Butembo.

Mambembe ni kata inayo patikana katika mji wa Mangurudjipa usulutani wa baswagha wilayani lubero Kivu kaskazini mashariki mwa DRC, eneo hilo limeshuhudia wasiwasi baadha ya kushambuliwa na watu wanao dhaniwa kuwa ADF usiku wa juma tano tano 7 mei 2025.

Hali ambayo imesababisha maandamano ya vijana wa eneo hilo wakiomba viongozi wa serikali na wale wa muungano wa jeshi la Uganda UPDF na FARDC kuwa na uzembe katika ulinzi wa Mji huo japo jeshi hilo lilikuwa lime fanikiwa katika msako wa wapiganaji hao katika vijiji mbali mbali pembezoni mwa Mji wa Mangurudjipa huku muwakilishi wa serikali anae kuwa na makao yake pa Djiapanda alishambuliwa na kupigwa makofi na vijana wenye hathira baada ya kuokolewa na wanajeshi tiifu kwa serikali FARDC.

Taaarifa za sasa zasema mtu mmoja alifariki Dunia kwakuwawa kwa shoka Pamoja na pikipiki kuchomwa moto na Pamoja na pikpiki zikishambuliwa watu wanao dhaniwa kuwa ADF, ADF ambao wana shutumiwa kwaa vitendo vya kigaidi kwa muda mrefu enela Mangurudjipa, walio jeruhiwa kwa mapanga wakiwa wamefikishwa hospitalini kwa ajili ya tiba.

Hadi tukienda hewani jeshi la serekali limeanzisha msako katika misitu na shamba kwani eneo hizo zina misiti Zaidi, huku idaidi kamili ya maafa bado ikiwa.

Huku Shirika la kiraia la secta la Bapere kupitia muratibu wake Kakule kagheni Samuel aomba viongozi wa kiserekali hasa wakuu wa Mkoa ambao wame weka ngome yao katika Mji wa Beni kutembelea Mangurudjipa.

Utafahamu kwamba mauji hayo yameshudiwa week tatu baada ya mapambano kulipuka kati ya makundi mawili ya wazalendo katika Kijiji cha kaheku karibu na kata hilo kwenye barabara Butembo Manguredjipa na kupelekea usafiri kusimamishwa Mara Nyingine. Serikali ikombwa kutafuta suluhisho kuhusu swala la wazalendo.

Abel Tsongo MTV1 online