DRC

Watu ambao idadi yao kamili haijulikane wame uwawa na wengine kutekwa na ADF Mambasa mkoani Iruri

APRILI 02, 2026
Border
news image

Baadhi ya wakaazi wa vijiji mbali mbali wilayani Mambasa Mkoani Ituri wameshindwa kuvumilia hali ya ukosefu wa usalama ambao kwa sasa umekita mizizi, hasa mauaji na utekaji nyara kutoka kwa watu wanaodhaniwa kuwa ADF wanaopatikana katika misitu ya Mambasa, Beni na Lubero kwa muda mrefu.

Kisa cha hivi karibuni kikiwa katika eneo la kilometa Bafako kwenye umbali wa zaidi ya kilometa mia moja arobaini na nane, ambako wakaazi wengi wameuawa, makaazi kuchomwa moto na wengine kutekwa na watu wanaodhaniwa kuwa ADF.

Wakaazi wengi wamekimbilia misituni na wengine kushikwa na hofu na kuonekana kuchoka kulalamika kwa kutuma ripoti kwa viongozi. Paluku, mkuu kiongozi wa shirika la raia, amesema kwa sasa wameshindwa kuelewa msimamo wa serikali ya Kinshasa kutokana na mauaji pamoja na mashambulizi ya ADF.

ADF imeanza kuwaua watu kwa zaidi ya miaka kumi sasa chini ya uangalizi wa Umoja wa Mataifa kupitia MONUSCO na katika uangalizi wa serikali kuu ya Kinshasa, bila mafanikio makubwa katika operesheni za kijeshi.

MTV1 Online