DRC - Lubero/Manguredjipa

Watu Wafariki na Nyumba Kuchomwa Moto Wakati wa Sherehe za Mwaka Mpya Mangurudjipa

JANUARI 02, 2026
Border
news image

Watu abao idadi yao kamili haijulikane wafariki Dunia na nyumba kuchomwa moto katika shambulizi la watu wanao dhaniwa kuwa ADF wakati wa sherehe za mwaka mpya katika mji wa Mangurudjipa wilayani Lubero Kivu Kaskazini mashariki mwa Congo.

Taarifa za sasa zasema milio ya silaha nzito zilisikika Alhamisi mosi Januari elfu mbili ishirini na sita katika kata ya Mangurudjipa karibu na kambi ya wanajeshi wa Uganda (UPDF) walioko eneo la Secta ya Bapere wilayani Lubero, hali iliyosababisha wasiwasi mkubwa miongoni mwa raia waliokuwa wakisherekea sikukuu za mwaka mpya.

Wakaazi wa kata ya Katanga walishindwa kutoroka makaazi yao kutokana na milio ya silaha nzito iliyosababisha vifo na maafa ambayo hadi sasa idadi yake haijajulikana. Mkaazi mmoja aliyezizungumza na MTV amesema jirani yake mmoja alifariki Dunia kwa presha kutokana na milio ya risasi, huku watu wengine wawili wakijeruhiwa, pamoja na nyumba kuchomwa moto.

Eneo hili limeshuhudia maafa makubwa na matukio mabaya mara kwa mara kutokana na mashambulizi ya watu wanaodhaniwa kuwa ADF. Secta ya Bapere ipo wilayani Lubero, Kivu Kaskazini magharibi mwa mji wa kibiashara wa Butembo, ambako kuna majeshi ya Uganda (UPDF) na Congo (FARDC) yanayoendesha msako dhidi ya ADF. Kundi hilo linashutumiwa kwa vitendo vya uhalifu wa kivita, ikiwemo mauaji, uporaji na uchomaji wa nyumba za wakaazi wa Lubero, Beni na sehemu za Mkoa wa Ituri kwa zaidi ya miaka kumi na tano hadi sasa.

Abel Tsongo - MTV1 Online